Ligi Kuu soka Tanzania bara
msimu wa 2016/2017 iliendelea tena Alhamisi ya October 20 2016 kwa wekundu wa
Msimbazi Simba waliwaalika Mbao FC ya Mwanza kucheza
mchezo wao wa 10 Ligi Kuu Tanzania bara
uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Mchezo wa Simba na Mbao FC umekuwa tofauti na ulivyokuwa unatarajiwa na wengi kuwa Mbao wangeweza kuruhusu magoli mengi kwa Simba kutokana na Simba kwa sasa wanafanya vizuri wakati Mbao FC wakiwa wageni katika Ligi Kuu.
Hali ya mchezo ilizidi
kuwa ngumu kwa pande zote mbili kutopata matokeo, hali ambayo ilimfanya kocha
wa Simba Joseph Omog kufanya mabadiliko yaliozaa matunda kwa
kumtoa Laudit Mavugo na kumuingiza Fredrick Blagnon aliyetoa pasi ya goli lililofungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 86 na kuufanya mchezo kumalizika
kwa Simbakuibuka
na ushindi wa goli 1-0.