Wakati magazeti ya leo yakitoka
na habari iliyosema kuwa wanafunzi wa vyuo 66,000 kukosa mikopo, taarifa hizo
zilidai kuwa wanafunzi 88,000 walioomba mikopo kutoka bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu, wengi hawatapata.
Taarifa hizo zilizochapishwa na
gazeti la mwananchi la October 20 2016 zimesema kuwa uwezo wa bodi hiyo ni
kutoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliopatiwa hadi
sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na asilimia 12.
Wakati hayo yakielezwa leo
October 20 2016 baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wakiongozwa
na viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho ‘DARUSO’ wamefika Wizara ya
elimu wakiwa na hoja kuu mbili, uchache wa majina ya wanuafaika wa mikopo
yaliyotoka mpaka hivi sasa na hoja ya pili ni kuhusu vigezo ambavyo
vimetumika kwenye fedha ya kujikimu kwa wanafunzi.
Hata hivyo baada ya kufika
wizarani hapo wanafunzi hao wamesema hawakupata nafasi ya kumuona waziri wa
elimu lakini wamefikisha hoja zao kwa katibu mkuu wa wizara na ametoa ahadi ya
kushughulikia hoja hizo.