Leo October 28, 2016 zimetajwa nchi 140 zenye watu wakarimu zaidi duniani. Na Tanzania imetajwa humo pia japo nafasi yake ni ya chini ikipitwa na nchi kama Kenya ambayo imekamata nafasi nafasi ya 12 kwenye orodha ya takwimu za mwaka 2015 huku nchi ya Myanmar ambayo zamani ilikua ikiitwa Burma ikiongoza.
Nchi ya Myanmar ilifanikiwa kushika nafasi hiyo pia mwaka 2015 ikiiacha nyuma Marekani ambayo iliongoza mwaka 2014. Tanzania imetajwa kwenye nafasi ya 57 na Uganda ikiwa nafasi ya 26.
Kwa mujibu wa shirika la Charities Aif Foundation ambalo hutayarisha orodha nzima, imesema kuwa list hiyo huzingatia uwezekano wa watu kuwasaidia wageni, watu kutoa pesa za kusaidia wengine na watu kujitolea muda wao kuwasaidia wengine.
Kwenye orodha hiyo, ambayo hutayarishwa na shirika la Charities Aid Foundation, nchi ambazo raia wake waliwasaidia wageni kwa urahisi ni nchi ambazo zinakabiliwa na mizozo ya kivita.
Hapa nimekuwekea list nzima ya nchi zenye watu wakarimu duniani.