Kama ni Rahisi Kununua Tuzo, Wanaosema Hivyo na Wao Wakanunue – Babutale - HABARI TANZANIA

Post Top Ad

Wednesday, 19 October 2016

demo-image

Kama ni Rahisi Kununua Tuzo, Wanaosema Hivyo na Wao Wakanunue – Babutale

Responsive Ads Here
tuzoo
Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.

Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.

Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.

Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.

Post Bottom Ad