Federer amshinda Nadal Shangai Masters - HABARI TANZANIA

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 16 October 2017

Federer amshinda Nadal Shangai Masters

Ni Jimmy Connors pekee ndio ameshinda michezo mingi zaidi ya Federer 1971-88Ni Jimmy Connors pekee ndio ameshinda michezo mingi zaidi ya Federer 1971-88
Bingwa mtetezi wa Wimbledon Roger Federer amemshinda mchezaji namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal kwa seti 6-4 6-3 katika michuano ya Shanghai na kuwa kikombe chake cha sita kwa mwaka huu.
Federer ambaye amepoteza michezo minne tu kwa mwka 2017, alikuwa katika kiwango cha juu na kushinda ndani ya dakika 72.
Ulikuwa ushindi wake wa nne kwa mwaka huu dhidi ya Nadal na wa sita mfululizo.
Federer ameshinda mataji 94 katika maisha yake ya uchezaji tenisi huku 19 ikiwa ni grand slam.
Inamfanya kufikia rekodi ya Ivan Lendl wakipitwa na Jimmy Connors wa Marekani mwenye vikombe 109.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here