Mahakama ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam leo imemfutia shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete maarufu kwa jina la Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani hapo kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Salum Njwete maarufu kama
‘Scorpion’ anayetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho
amefikishwa mahakama ya Ilala Dar es salaam leo na kusomewa shitaka la
unyang’anyi kwa kutumia silaha.Upande mashitaka
uliiomba mahakama kuliondoa shitaka la unyanganyi wa kutumia silaha
linalomkabili Salumu Njwete kwa nia ya kutotaka kuendelea nalo.Kutokana na ombi
hilo hakimu Adelf Sachole alikubaliana na ombi hilo kuliondoa shitaka hilo
kupitia kifungu cha 91 (1) ambapo kinampa mamlaka mkurugenzi wa mashitaka (DPP)
kuondoa mashitaka muda wowote ilimradi isifike kwenye hukumu.
Baada ya saa kadhaa
alifunguliwa shitaka hilohilo tena la unyang’anyi kwa kutumia silaha
alilolifanya September 6 2016 Buguruni sheli Dar es salaam na jumla ya
vitu alivyochukua 476000 kwa hakimu mwengine Frola Haule. Salumu alikana
mashitaka hayo.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani anatuhumiwa kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa Mabibo Hostel hivi karibuni.