Ujumbe wa mfalme wa Oman wawasili Zanzibar - HABARI TANZANIA

Post Top Ad

Friday, 13 October 2017

demo-image

Ujumbe wa mfalme wa Oman wawasili Zanzibar

Responsive Ads Here
_98295385_0851c0c9-a626-4f16-927b-85a96e0b4f36
Ujumbe wa watu 300 ambao wanawakilisha mfalme wa Oman Sheikh Sultan Qabous bin Said siku ya Alhamisi , uliwasili mjini Zanzibar ukiabiri meli kwa jina Fulk Al l Salamah' inayotumiwa na familia ya ufalme huo.
Ujumbe huo uliotoka Muscat Oman uliwasili katika bandari ya Malindi na kupokewa na makamu wa rais wa pili Seif Ali Idd ambaye aliandamana na mawaziri wanne.
Ujumbe huo wa Oman uliongozwa na waziri wa mafuta na gesi Mohammed Al-ramh.
Ziara hiyo inalenga kuhimiza amani na umoja duniani.
Akizungumza katika hafla hiyo, waziri katika afisi ya makamu wa rais wa pili Mohammed amesema kuwa ziara hiyo ni muhimu kwa serikali ya Zanzibar.
Amesema kuwa inafungua ukurasa mpya kuhusu ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili yalio na historia ndefu.
Waziri huyo amesema kuwa ujumbe huo pia utapewa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na afisi za serikali ili kubadilishana mawazo kuhusu ukuwaji wa kiuchumi.

Post Bottom Ad