Siku nne baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africansmuholanzi Hans van Pluijm ajiuzulu nafasi yake hiyo, leo October 28 2016 klabu ya Yanga imemuandikia barua ya kumuomba abadili maamuzi yake ya kujiuzulu na arejee kazini kama kawaida.
Baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake Baraka Deusdedit pamoja na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ambaye pia ni shabiki wa Yanga na mwanachama, wamemuomba kocha Hans van Pluijm atengue uamuzi wake wa kujiuzulu na kurudi kazini kama kawaida.
Kwa maamuzi hayo ya Yanga kumuomba kocha Hans van Pluijm arudi usishangae ukimuona akirejea katika benchi la Yanga kwa siku za karibuni, inaripotiwa kuwa maamuzi ya Yanga kuandika barua hiyo yaliafikiwa baada ya kukaa na kufanya maongezi na kocha Hans van Pluijm kwa siku tatu pamoja na katibu na waziri Mwigulu.