Jina la Luis Suarez wa FC Barcelona limegonga headlines tena baada ya kuripotiwa na mtandao wa ESPN kuwa Suarez anaamini hawezi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or huku akitaja baadhi ya sababu zake.
Suarez amesema hayo baada ya kukabidhiwa kiatu cha dhahabu na wengi wakihoji baada ya tuzo hiyo ya ufungaji bora wa Laliga mwaka 2015/2016 vipi anaweza akapewa nafasi ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya?
“Ballon d’Or ipo kwa ajili ya masuala ya biashara yaani mtu anayefanya vizuri zaidi sokoni kuliko mafanikio ya uwanjani, nimeshinda tuzo zote ikiwemo ya ufungaji bora hiyo huwa haina ubishi kwa sababu anapewa mtu aliyefunga magoli mengi hivyo hiyo mtu hawezi kuninyima, Ballon d’Or inaangalia mtu anayeuza mimi siuzi malengo yangu ni kushinda Champions League kwa sasa”