Shirika la Fedha Duniani IMF limetoa ripoti yake kuhusu hali ya ukuaji wa uchumi katika nchi za eneo la chini ya jangwa la Sahara barani Afrika ambapo inaonesha kuwa Uchumi unatazamiwa kupungua kwa kiasi kikubwa ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 20.
Ripoti ya IMF imesema uchumi katika eneo hilo unatazamiwa kustawi kwa kiwango cha asilimia 1.5 mwaka huu, kutokana na mfumko wa bei za bidhaa sambamba na mazingira mabaya ya kiuchumi duniani.
Hata hivyo ripoti hiyo imebainisha kuwa, uchumi wa nchi kama Kenya, Ethiopia, Ivory Coast na Senegal ambazo hazina maliasili, zinafanya vizuri kutokana na marekebisho katika sekta ya miundombinu na vile vile kuagiza mafuta kwa bei ya chini.
Aidha ripoti ya IMF imesema kuwa, Uchumi wa nchi zinazoagiza bidhaa kama Angola, Nigeria na Afrika Kusini unayumba kutokana na kuporomoko kwa bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa.soma zaidi